Moja ya Couple maarufu katika tasnia ya Bongo Fleva, Aika na Nahreel wanaounda kundi la Navy Kenzo, wameshare na mashabiki wao ugomvi wao mkubwa kwa mwaka 2015, chanzo kikiwa ni kurekodi vesi katika ngoma yao ya Game.
Akiongea na eNewz, Aika ameeleza kuwa, aligombana na Nahreel mpenzi wake huyo kukataa vesi zake katika rekodi ya game, ambapo alilazimika kurudia kufanya mara tatu, na baada ya hapo pia kulazimika kuifanya tena baada ya kukamilisha kupiga picha za video yake. Aika anasema kuwa, ugomvi huo ulizimwa baada ya rekodi yenyewe kufanya vizuri, akieleza kuwa kama ingekuwa vinginevyo, wangekuwa wamenuniana mpaka sasa.
Kwa upande wa Nahreel amesema kuwa, mara nyingi anakuwa mkali kwa mpenzi wake huyo kutokana na kupenda kufanya kazi nzuri ambayo mara kwa mara husababisha kumkaripia mpenzi wake pale anapoona kuwa amefanya kitu isivyo sawa, yote ikiwa ni kwa nia ya kufanya kazi nzuri.
Enews.
EmoticonEmoticon