Wednesday, May 25, 2016

Hamisa Mobetto Looking Lovely with Strong Message For Ladies " Mwanamke Anayejielewa"


Have Ever Though Of Being Addressed That Way  Well According to Model Hamisa Mobetto, She Penned Down This Long Message to Help You Ladies Out There To Know Were Do You Stand...

Read It Below:-  " Mwanamke Anayejielewa Ni Yule Anayetambua Uwepo Wa Hekima Kwenye Kila Anachokifanya Na Mahali Popote Pale. Mwanamke Anayejielewa Ni Yule Anayeonyesha Ushupavu Kwenye Maisha Yake Ya Kila Siku Hasa Pale Anapopatwa Na Matatizo MbaliMbali.

 Mwanamke Anayejielewa Ni Yule Asiyekata Tamaa Pamoja Na Kusakamwa Na Kila Aina Ya Watu Kwa Mambo Yasiyo Na Mbele Wala Nyuma. Mwanamke Anayejielewa Ni Mnyenyekevu Kwa Jamii Bila Kujali Huyu Ni Mkubwa Au Mdogo, Anaheshimu Kila Mmoja Kwa Nafasi Yake. Mwanamke Anayejielewa Hawezi Kuwa Ni Mtu Wa Majungu, Umbea Wala Fitina Kwa Wengine, Muda Wake Huutumia Kusaka Pesa Na Kuangalia Familia. 

Mwanamke Anayejielewa Ana Msimamo Na Anaelewa Afanye Nini Muda Gani Na Kwa Nani, Anajua Nini Asifanye Na Kwanini. Mwanamke Anayejielewa Hatajiangalia Sura Tu Au Kwamba Amejazia Sana Au Labda Anajua Sana Kwenda Na Wakati. Mwanamke Anayejielewa Lazima Awe Na Roho Nzuri Kwa Wengine, Ukarimu Na Ucheshi Bila Kuangalia Ni Nani Anamfanyia Yote Hayo.💙 "

There Now You Know...Wewe ni Wa Design Gani.... Thanks Hamisa.


EmoticonEmoticon